MBEYA UNIVERSITY OF SCIENCE AND TECHNOLOGY
ONLINE BILLING AND INVOICING SYSTEM
February 03,2026
View Training/Event Information
Training/Event Name : MAFUNZO YA UJASILIAMALI KWA VITENDO
Location/Venue : JENGO JIPYA LA CITT- CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA - KAMPASI KUU
Duration : 06-02-2026 - 08-02-2026
Training/Event Fee : 25,000.00
Training/Event Description

Kozi ya Mafunzo ya Ujasiliamali kwa Vitendo ya siku tatu inalenga kuwajengea washiriki ujuzi wa vitendo na maarifa ya uzalishaji ili kuwawezesha kuanzisha na kuendesha shughuli za kijasiriamali. Mafunzo yanazingatia utengenezaji wa bidhaa zinazohitajika katika matumizi ya kila siku pamoja na bidhaa za ubunifu, kwa lengo la kuongeza ajira binafsi na kipato.

Katika siku mbili za mwanzo, washiriki watapata mafunzo ya vitendo ya utengenezaji wa sabuni za vipande kwa matumizi ya kuoshea vyombo, kufulia na kuogea, utengenezaji wa shampoo na shower gel, pamoja na utengenezaji wa batiki na vijora vya aina mbalimbali. Mafunzo yatahusisha matumizi sahihi ya malighafi, hatua za uzalishaji, udhibiti wa ubora, usalama kazini, na mbinu za kufungasha bidhaa tayari kwa soko.

Siku ya tatu itajikita katika elimu ya ujasiriamali na masuala ya kifedha, ikihusisha elimu ya mikopo kutoka taasisi za fedha, aina na masharti ya mikopo kwa wajasiliamali, pamoja na taratibu za kuomba mikopo hiyo. Aidha, washiriki watapata misingi ya uendeshaji wa biashara ndogo, usimamizi wa fedha na mikakati ya kukuza biashara zao ili kufanikisha kujitegemea kiuchumi.

Yaliyomo Katika Kozi / Mada za Kozi:

Ø  Utengenezaji wa Sabuni za vipande kwa matumizi ya kuoshea vyombo, kufulia na kuogea.

Ø  Utengenezaji wa batiki na vijora aina zote.

Ø  Utengenezaji wa shampoo na showergel.

Ø  Elimu ya mikopo kutoka taasisi za fedha itatolewa ikiwemo utaratibu wa kupata mikopo hiyo kwa wajasiliamali.

Kikundi Kinacholengwa / Washiriki Waliolengwa:

Wanafunzi, Wafanyakazi, Wajasiliamali wadogo Pamoja na jamii inayotuzunguka MUST.

 Malengo ya Kujifunza:

Baada ya kukamilisha mafunzo haya ya siku tatu, washiriki wanatarajiwa kuwa na uwezo wa:

Ø  Kutengeneza kwa vitendo sabuni za vipande, shampoo, shower gel, batiki na vijora vya aina mbalimbali kwa kuzingatia ubora na usalama.

Ø  Kutambua na kutumia malighafi sahihi pamoja na mbinu bora za uzalishaji, ufungashaji na uandaaji wa bidhaa kwa soko.

Ø  Kuanzisha na kusimamia biashara ndogo kwa kutumia misingi ya ujasiriamali na usimamizi wa fedha.

Ø  Kuelewa aina za mikopo inayotolewa na taasisi za fedha, masharti yake na taratibu za kuomba mikopo kwa wajasiliamali.

Ø  Kuandaa mpango rahisi wa kukuza biashara na kutumia fursa za kifedha ili kuongeza kipato na kujitegemea kiuchumi.

Wawezeshaji Mafunzo:

-Dr Ukende Kingu

-Mr Ezekia Laiton

-Mr Joseph Kihongole

KWA MAWASILIANO ZAIDI:

-          TUPIGIE : +255 717 216 565 / +255 670 7455 92 / +255 754 957 243

Deadline for Registration :: Thursday Feb 05 2026
Registration Information

REGISTER AS ORGANISATION